Brazil jana imetangaza kuruhusu kuanza tena kwa safari za ndege za kimataifa kwa watalii wa kigeni tangu ilipozifuta mnamo mwezi Machi kutokana na janga la virusi vya corona.
Amri iliyotolewa na serikali imesema watalii kutoka mataifa yote duniani wanaweza kuitembelea nchi hiyo kama watakuwa na bima ya afya ya kipindi chote cha safari.
Nchi hiyo ya Amerika ya kati iliyoathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona hajifafanua zaidi kuhusu sababu za kufikia uamuzi huo katika wakati inashika nafasi ya pili nyuma ya Marekani kwa idadi ya vifo na maambukizi ya COVID-19.
Hapo jana serikali ilitangaza vifo vingine 1595 vya COVID-19 na idadi hiyo imekuwa ikipanda kwa wiki ya tano mfululizo huku maambukzi yakisambaa kwenye majimbo mengine nchini humo.
Brazil inafungua mipaka yake haraka kuliko mataifa mengine ya kanda hiyo yenye idadi ndogo ya maambukizi kama Colombia, Argentina, Panama na Peru ambayo bado yamezuia safari za ndege za kimataifa
No comments:
Post a Comment