![]() |
| Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Benki ya NMB, Eunice Chiume, akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari katika Banda la NMB lililopo viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Wafanyakazi wa Benki ya NMB katika picha ya pamoja ndani ya Banda la NMB, Saba Saba jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano na waandishi wa habari. |
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Benki hiyo - Eunice Chiume, amesema Benki ya NMB inashiriki kimkakati zaidi, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kibenki zikiwemo kuweka na kutoa pesa/ kubadilisha fedha hata za kigeni, kuwahamasisha na kuwaelimisha Watanzania kuhusu umuhimu wa huduma za kibenki na shughuli za kifedha katika maendeleo ya mtu binafsi, taasisi na taifa kwa ujumla.
“Kwa ufupi, tunaweza kusema kuwa Benki ya NMB imehamia Saba Saba kwani huduma zetu zote za kibenki na nyingine mbalimbali zinapatikana kwenye banda letu. Kuwepo kwetu hapa ni zaidi ya kujitangaza kwani pia tunataka kuwaonyesha Watanzania jinsi huduma zetu mbalimbali zikiwemo zile mpya kama za bima zinavyochangia kwenye ukuaji wa uchumi” Bi. Eunice Alisema.


No comments:
Post a Comment