Dar es Salaam, Julai 3,2020 - Benki ya ABC (BancABC) imeshiriki maonesho ya 44 ya biashara maarufu kama Sabasaba ambapo benki hiyo imeeleza namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za kibenki hasa utoaji wa mikopo nafuu kwa wateja wake.
Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Akizungumza kwenye maonyesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha hazina wa benki hiyo, Barton Mwasamengo alisema benki imejidhatiti katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wengi kwa kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.
“Tunatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na mikopo binafsi kwaajili ya kuendeleza shughuli ndogondogo kama mamalishe, boda boda na wengine wengi, BancAbc ipo kwaajili ya watanzania wote,” alisema Mwasamengo.
Mwasamengo alisema katika kuboresha huduma imefanikiwa kutoa huduma za kibenki za kidigitali ambapo wateja wanaweza kufanya malipo mtandaoni kwa urahisi zaidi.

No comments:
Post a Comment