Mchakamchaka wa kuomba ridhaa Ndani ya Chama Cha mapinduzi kwa nafasi ya ubunge na udiwani umefunguliwa huku zaidi ya wagombea ubunge 30 wakijitokeza kwa nyakati tofauti kuchukuwa fomu katika Jimbo la Arusha mjini
Akizungumza wakati wa Zoezi la kuchukuwa fomu katika makao makuu ya Chama hicho wilayani hapa Katibu wa CCM Wilaya Arusha Denis Mwita Zakaria amesema kuwa uchukuaji wa fomu utaenda sambamba na maagizo ya Chama kwa Kila mmoja kufuata taratibu.
Alisema kuwa msingi na maadili ya Chama hicho kwa wagombea hadi kwenye siku ya mchujo yahitajika kuzingatiwa kwa waombaji wote Ndani ya CCM hivyo kila moja anao wajibu wa kufuata maagizo hayo ikiwemo kutotoa rushwa Wala kuanza kampeni mapema.
"Niwaombe Sana wagombea kuendelea kuchukuwa fomu na kusubiria maelekezo ya Chama kwa kufuata utaratibu kanuni na maadili kwa wagombea wote ikiwemo kukwepa vitendo vya rushwa wakati wote wa uchaguzi wa Ndani ya Chama hicho pamoja na kutochezeana rafu"
Awali baadhi ya wagombea akiwemo meya mstaafu wa jiji la Arusha Kalist Lazaro aliyechukuwa fomu mchana alisema kuwa ametumia haki yake ya kikatiba kuchagua na kuchaguliwa ndio vilivyomsukuma kuomba nafasi hiyo.
Nae Mrisho Gambo alisema kuwa Kuna mengi yanamsukuma kuomba nafasi hiyo hivyo watu wasubiri muda utaongea hapo usoni kwani ana imani na vikao vya Chama hicho kuweza kuleta mgombea anayekubalika atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika Jimbo la Arusha.
Kwa upande wake Philemon Mollel alisema kuwa anayoimani kubwa ndio maana akaamua kuchukuwa fomu kuomba Chama hicho kumpitisha kugombea nafasi hiyo hivyo wasubiri vikao kwa Sasa Sina zaidi ya haya.
Katika ofisi za Wilaya ya Arusha za Chama hicho wagombea kadhaa wamekuwa wakipishana kuchukuwa fomu za kuomba Chama hicho ridhaa ya kupata nafasi ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.
Hatua hiyo inaleta kuwepo kwa mvutano mkubwa wakati wa kura za maoni na kukifanya Chama hicho kuweza kumpata mgombea atakayekwenda kupambana na mgombea wa vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu mwezi November.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Arusha mjini ambaye ni Mwanamama wa kwanza kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo Hilo Anna Mwambapa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Arusha mjini leo kutoka kwa katibu wa Chama Cha Mapinduzi Denis Mwita ,mgombea huyo alisindikizwa na familia yake kwenda kuchukuwa fomu katika ofisi za CCM Wilaya zilizopo Wilaya ya Arusha (picha na Woinde Shizza,ARUSHA)
Mfanyabiashara Maarufu jijini Arusha Philemon Mollel (Monabani) akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha mjini na katibu wa CCM Wilaya ya Arusha mjini Denis Mwita
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi Victor Mollel fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Arusha mjini .
No comments:
Post a Comment