Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na viongozi wa Dini na Viongozi mbalimbali pamoja na wanahabari wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambae pia ni Shekh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza wakati wa mkutano huo
Viongozi wa Dini kupitia Jumuiya ya Maridhiano Tanzania kwa kauli moja leo wamempongeza Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa namna alivyomtanguliza Mungu mbele katika Mapambano dhidi ya Corona ambapo pia wamelipongeza Bunge la Tanzania kwa msimamo wao wa Kumpongeza Rais.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambae pia ni Shekh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum amesema mbali na kumpongeza Rais kwa kusimama imara kuhakikisha makanisa na Misikiti havifungwi pia wanaunga mkono kwa asilimia mia moja juhudi anazofanya katika kuliletea Taifa Maendeleo.
Akizungumza katika Kikao hicho Sheikh Mussa amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa namna anavyoendesha Mkoa huo jambo linalofanya hali ya amani na utulivu kuwa shwari.
No comments:
Post a Comment