Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brig. Marco Gaguti, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwaimu, Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mh. Godfrey Muheruka, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine na mwenyekiti wa chama cha KDCU LTD Anselemi Alphonce.
Benki ya wakulima (TADB) ikiongozwa na Mkurgenzi Mtendaji, Japhet Justine, wameshiriki katika ufunguzi wa msimu mpya wa kahawa 2020/21 uliofunguliwa na RC Kagera Mh. Brig. Gaguti wilayani Kyerwa jana Jumanne.
‘TADB inaendelea kuwa mdau mkuu wa wakulima tangu msimu 2018/19 tulipoanza kwa kuwekeza bil 30 na bil 23 kwa msimu 2019/20 na kutokana na kufanya vizuri, Oct 2019 tuliwatembelea na kutunuku pikipiki kwa vyama vya Luicho na Nyakatuntu’ amesema Mkurugenzi Mtendaji Japhet Justine
Amesema TADB imeleta mapinduzi kwa wakulima 142,000 na kuendelea kuhamasisha wakulima kujiunga na vyama na kufungua benki akaunti na mpaka sasa wanalipwa kupitia benki
Amesisitiza kwamba kwa vile Serikali ya awamu ya 5 inahimiza na kudhamiria maendeleo ya moja kwa moja kwa wakulima wadogo, hivi sasa TADB imeshusha riba kutoka 12% hadi 9% yote hayo kutokana na uaminifu wenu na punguzo hili litapunguza gharama na kuongeza tija kwa wakulima
"Wakati tunaanza vyama vilikuwa na madeni makubwa hadi bil 7, mpaka sasa KDCU hawana deni na KCU wanamalizia. Hivyo tungependa vyama visimame na vijiendeleze vyenyewe kwa ufanisi. Tunahitaji kuviwezesha vyama hivi kwa maendeleo ya uchumi wa wakulima", aliongeza Mkurugenzi Mtendaji wa TADB.
Mkoa wa kagera unazalisha 68% ya ndizi nchini, na kahawa 45% ilitoka Kagera na tulikusanya kilo million 52 na kuzalisha billion 84, ikiwa malengo ya msimu huu ni kukusanya kilo million 60. Tunajivunia kwamba mwaka huu hakukuwa na changamoto kama miaka mingine, kulikuwa na utulivu hivyo tunaomba wakulima waendele kufata kanuni bora za kilimo pamoja na kutumia mizani ya kidijitali. Asisitiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Aidha, Bw. Oscar, Meneja KDCU amesema msimu mpya wa 2020/21 vyama vitanunua kahawa kwa wakulima kiasi cha shilingi 1200/- kwa kilo ikiwa ni ongezeko kutoka 1100 msimu uliopita. Bei hii ina tija kwa wakulima kwani soko la dunia bei ni sh. 850 hadi 867, Asante sana TADB kwa kuwezesha hili.
No comments:
Post a Comment