Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wakazi wa mbagala alipofanya ziara yakukagua miradi mbalimbali iliyotelekezwa na Raisi Magufuli katika Wilaya ya Temeke leo jiji humo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikagua mitaro inayojengwa katika shule ya sekondari Kibasila ambayo imekuwa korofi wakati wa kipindi cha mvua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizindua Majengo ya Madarasa
124, Matundu 124 ya Vyoo na Madawati 7,179 kwenye Shule ya Sekondari Mbagala na
Shule nyingine 16 Wilayani humo jambo linalokwenda kusaidia zaidi ya Wanafunzi
5,000 waliofaulu na kukosa nafasi kupata uhakika wa kuendelea na masomo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda amemuelekeza Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es
salaam kuhakikisha wanawashughulikia ipasavyo baadhi ya vijana walioanza tabia
ya kupora na kuiba Mali za Watu jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya Watu.
RC Makonda amesema operesheni
maalumu ya kushughulikia Vibaka hao imeanza rasmi jana ambapo amemtaka kila
mzazi kuhakikisha anamchunga mwanae kwakuwa hakuna kibaka atakaesalimika katika
msako huo.
Mhe. Makonda ametoa
agizo hilo wakati wa Ziara ya ukaguzi miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke
iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Majengo ya Madarasa 124, Matundu 124 ya Vyoo
na Madawati 7,179 kwenye Shule ya Sekondari Mbagala na Shule nyingine 16
Wilayani humo jambo linalokwenda kusaidia zaidi ya Wanafunzi 5,000 waliofaulu
na kukosa nafasi kupata uhakika wa kuendelea na masomo.
Aidha RC Makonda
ametembelea Ujenzi wa kituo cha Afya Buza na Hospital ya Yombo Vituka yenye uwezo
wa kuhudumia wagonjwa 2,000 kwa Siku ambapo amesema kuongezeka kwa Zahanati,
Vituo vya Afya na Hospital vinakwenda kurahisisha upatikanaji wa Huduma za
Afya kwa wananchi.
Pamoja na hayo RC
Makonda amesema ifikapo Juni 20 ataanza Ziara ya Siku 10 na Kamati ya Siasa ya
Mkoa kwenye kila jimbo kwa lengo la kukabidhi miradi iliyokamilika ikiwa ni utekelezaji
wa Ilani ya CCM kwa Vitendo.
Katika Ziara hiyo RC
Makonda pia ametembelea *Ujenzi Mitaro yenye urefu wa Km 9 Wilayani humo
ikiwemo mtaro mkubwa kabisa unaojengwa eneo la Serengeti kuelekea Shule ya
Sekondari Kibasila na Maradi na Mradi wa uwezeshaji wa vijana kupitia 10% ya
mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa
namna inasimamia miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment