Vladimir Putin, rais wa Urusi azungumza na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel kuhusu hali inayoemdelea nchini Libya.
Taarifa kutuko ikulu ya rais mjini Moscow zinafahamisha ya kwamba baada ya kuonekana kuwa nchini Libya mtafaruku unaendelea, rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza na kansela wa Ujerumani kuhusu hali inavyoendelea nchini Libya.
Urusi imesema kuwa inaipongeza Misri kwa mchango wake anotoa katika jitihada za kuimarisha usalama nchini Libya.
Katika mkutano uliofayika kuhusu Libya chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa ilifahamishwa kuwa mgogoro huo utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo ambayo yatapelekea kukomeshwa kwa mapigano.
Viongozi hao wamezungumza pia kuhusu hali iliopo Ukranina na hali inayoendelea nchini Syria.
No comments:
Post a Comment