Kibali cha kuungana kutoka kwa mamlaka husika tayari vimeshapokelewa
Benki ya NIC Bank Tanzania Limited (NIC) na benki ya Commercial Bank of Africa (Tanzania) Limited (CBA) imeshapokea vibali vyote kuungana na kuanza kutoa huduma kuanzia tarehe 8 mwezi Julai mwaka 2020 kama benki ya NCBA Bank Tanzania Limited.
Uunganaji utafanyika kwa kuhamishwa kwa mali na dhima zote kutoka kwenye benki ya CBA kwenda benki ya NIC.
Utekelezezaji wa uunganaji utakuwa kwa kuhamishwa kwa mali na dhima, ambazo zimekwisha idhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania na Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission). Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuungana taasisi mpya, benki ya NCBA Bank Tanzania Limited itachukua dhama zote, majukumu na haki zote za umiliki wa mali zilizohamishwa kutoka benki ya CBA Benki kwenda benki mpya ya NCBA Bank Tanzania Limited. Vile vile itapokea wateja na madeni yote yaliyopo katika benki ya CBA mpaka sasa.
Benki zote mbili za CBA na NIC ziko katika mchakato wa kuhitimisha masharti mengine kutoka kwa Mdhibiti.
Benki Kuu ya Tanzania imezipatia kibali cha kuungana mapema mwaka huu. Kibali kilitolewa katika barua iliyosainiwa tarehe 14 mwezi Februari mwaka 2020 na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dr Bernard Y. Kibesse.
Baada ya mchakato kukamilika benki ya NCBA Bank Tanzania Limited itakuwa benki ya daraja la 2 (Tier 2 Bank).
Benki ya NCBA Bank Tanzania Limited itakuwa sehemu ya kundi la makampuni la NCBA Group PLC ambalo liliundwa tarehe 1 mwezi wa Oktoba mwaka 2019 baada ya kupata kibali kutoka kwa Benki ya Kuu ya Kenya na Hazina ya Taifa ya Kenya kuidhinisha uunganaji wa makampuni ya NIC Group PLC (NIC) na Commercial Bank of Africa Limited (CBA).
"Jina la NCBA Bank linaashiria kuungana kwa benki mbili kubwa, benki ya NIC na CBA. Huu ni mwanzo wa safari mpya inayounganisha ubora wa benki zote mbili na kuunda taasisi kubwa na yenye nguvu zaidi ya kifedha na kuimarisha uchumi wa Tanzania". Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Commercial Bank of Africa (Tanzania) Limited, Gift Shoko alisema.
"Kama sehemu ya safari ya kuungana tutatumia mwezi ujao kukamilisha mchakato wa kuoanisha mifumo yetu ili wateja wetu waweze kufurahia huduma zisizo na usumbufu katika mtandao mtawi yetu nchini Tanzania. Mkakati wetu wa uzinduzi vile vile utajumuisha ubainishaji wa utambulisho wa kundi jipya la mabenki la NCBA Group , "Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Bank (Tanzania) Limited, Margaret Karume, amesema.
Kama sehemu ya ushirikiano wa kikanda wa NCBA Group, uunganishaji wa biashara nchini Rwanda ulikamilika mwanzo mwa mwaka huu. Pia kufika mwishoni mwa robo hii ya mwaka inatarajiwa pia kukamilika nchini Uganda
No comments:
Post a Comment