Na Vero Ignatus
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuzima tukio la kuozeshwa kwa mtoto wa miaka 12 ambapo tukio hilo limetokea Kata ya Msa wilaya ya Arumeru ambapo wazazi wake walitaka kumuozesha kwa mwanume huyo kwa tamaa ya mahari na mifugo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amesema hivi karibuni kumeibuka wimbi hususani watu wenye tamaa ya mahari kutumia kipindi hiki ambacho wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliopo likizo kutokana na ugonjwa wa corona kutumia fursa hiyo kuwaozesha wanafunzi au watoto wao kwa wanaume.
Kamanda Shana alisema katika Kata ya Msa wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wazazi wenye mtoto mwenye umri wa miaka 12 walitaka kumuozesha mtoto wao kwa mwanaume mmoja mkazi wa kata hiyo,kabla hawajafanikisha nia hiyo ovu jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kudhibiti tukio hilo.
Kamanda Shana alisema kuwa hadi sasa jeshi la polisi mkoani hapa wanamshikilia baba mzazi wa binti huyo pamoja na mwanume aliyetaka kumuoa mtoto huyo.
''Kwa bahati mbaya sana ,nasema mchezo huu mchafu unawashirikisha baadhi ya wazee wa kimila, viongozi wa serikali ngazi ya vitongoji,vijiji wenye tamaa ya fedha pamoja na mifugo''Alisema Kamanda Shana.
Aidha Kamanda huyo alisema kuwa jeshi la polisi kamwe halitakuwa na huruma kwa mzazi au mlezi yeyote ambae atamuozesha mtoto wake au mwanafunzi kwa sababu ya kutaka fedha au mali,kwani sheria itachukua mkondo wake.
Endapo yupo mtu yeyote aliyepokea mahari kwa mtoto au mwanafunzi ,au alikula pesa ya ushenga kwa kufanuikisha zoezi hilo ovu ataitapika!Nasema hakika watapelekwa jela,nasema kama endapo mwananchi wakawaida jirani ndugu na jamaa alikula chakula katika sherehe hiyo kitamtokea puani.Alisisitiza Kmanda Shana.
Kamanda Shana ametoa wito kwa kwa wananchi kuwa endapo watasikia mzazi anayetaka kufanya hivyo au wakihisi jambo kama hilo watoe taarifa haraka kwa jeshi la polisi kabla hayajawakuta makubwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana.
No comments:
Post a Comment