Na: Mwandishi wetu Dar es Salaam.
Chama cha Siasa cha Labour Tanzania (TLP) leo Juni 24,2020 kimetangaza rasmi kumuunga mkono Rais wa Jahuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi Mkuu wa Octoba mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za chama hicho zilizopo Magomeni Usalama Jijini Dar es Salaam wakati wa kusoma taarifa ya Maadhimio hayo Mwenyekiti wa Chama hicho Augustino Mrema amesema kuwa kwa kauli moja ya kizalendo Wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chama hicho wameamua kwa sauti moja kumuunga mkono mgombea wa chama cha Mapinduzi CCM Mh Dkt John Pombe Magufuli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 October 2020.
Amesema kuwa azimiao hilo lilifikiwa baada ya kutafiti, kudadisi na kujiridhisha pasina shaka yoyote juu ya kazi zinazofanywa na Rais Magufuli kuwa zimevunja rekodi zilizowekwa tangu enzi za mkoloni na zinaacha alama kubwa kwa kizazi hiki na kizazi kijacho zikipeleka Taifa kwa kasi kwenye Uchumi wa kati, sambamba na kudumisha Amani, Upendo na Mshikamano wa Taifa kwa ujumla.
“Ndugu Watanzania wenzetu, Ifahamike kuwa,azimio hili la kumuunga mkono Mh Dkt John Pombe Joseph Magufuli lilifikiwa baada ya kutafiti, kudadisi na kujiridhisha pasina shaka yeyote juu ya kazi zinazofanywa na Mh Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa zinavunja rekodi zilizowekwa tangu enzi za mkoloni, zinaacha alama kwa kizazi hiki na kizazi kijacho, zinalipeleka Taifa kwa kasi kwenye Uchumi wa kati, zinadumisha Amani, Upendo na Mshikamamo wa Taifa letu, na huu ndio ulikuwa mwanzao wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama chatu cha tarehe 04/05/2019 pamoja na maazimio mengine kikao kiliazimia kila mjumbe/mwanachama apitie nukta kwa nukta kazi zinazofanywa na Mh Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye Ardhi ya Taifa hili la Tanzania” Alisema Mrema.
Aidha Mrema amesema kuwa Chama cha TLP kinatoa fursa na kuwakaribisha watu wote wanaogombea nafasi za Ubunge na Udiwani kwenye Majimbo na Kata mbalimbali kote nchini kukiunga mkono Chama chao kwa kumsaidia Mh Rais kwa kumnadi kwa Wananchi kupitia jukwaa la “ Ugombea ”bila kujali Chama wanachotoka.
“Sisi TLP tunaamini kama Mgombea wetu wa Urais Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli atanadiwa na Wagombea wawili ( 2 ) katika kila Jimbo na Kata zote Nchini yaani yule toka chama chake cha CCM na wapili toka chama chetu cha TLP hakika ushindi atakaoupata utatikisa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” Alisema Mrema.
Ameongeza kuwa chini ya Uongozi imara wa Rais Magufuli ameweza kufanya na kuendeleza Miradi mikubwa ambayo haikuwahi kufanyika kwa kipindi cha miaka 35 huku jumla ya thamani ya Miradi yote ikifikia 41.2% ya Miradi yote ambayo ni karibu na nusu ya thamani ya miradi yote 182 yenye jumla ya $146bln

No comments:
Post a Comment