Bunge la Umoja wa Ulaya limeelezea kuunga mkono maandamano dhidi ya ubaguzi na matumizi ya nguvu ya polisi na kutoa wito kwa Umoja huo kukabiliana na ubaguzi katika mipaka yake.
''Wakati wa kikao maalum siku ya Jumatano kuhusu ubaguzi Miriam Dalli, mmoja wa wabunge hao alisema kuwa inawapasa kuhakikisha kuwa jamii zote na raia wote wako huru.
Aliongeza kuwa maisha ya watu weusi ni muhimu na kwamba ni lazima wasema wazi kuwa ubaguzi haufai. Ili kushughulikia ubaguzi barani Ulaya kwa upana, bunge hilo katika maazimio yake limeyataka mataifa ya Umoja huo kuondoa maagizo ya kutokuwa na ubaguzi yaliyoanzishwa na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya mwaka 2008 lakini hayajapitishwa kwasababu yanapaswa kukubaliwa na mataifa yote wanachama na baadhi yameibua wasiwasi kuhusu uhuru wa mataifa yao.
No comments:
Post a Comment