A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, May 15, 2020

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Markezi, Ardem Arioglu, akiwa ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa, ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mandhari ya nje, wakati akiwa ndani ya treni inayotumia umeme, alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishuka, ndani ya treni inayotumia umeme, wakatialipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR.
  • Asema umetoa ajira zaidi ya 18,000; utapunguza muda wa safari
  • Asema nguzo za umeme 154 kati ya 160 zimeshasimikwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kusema kuwa mradi huo umesaidia kupungua tatizo la ajira kwa kuajiri wafanyakazi 18,700.

“Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huu, kumesaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwa kutoa ajira 7,400 kwa kipande cha Dar hadi Morogoro. Kipande cha Morogoro hadi Singida kimetoa ajira 6,300 wakati mradi wa umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere nao pia umetoa ajira 5,000,” amesema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema hayo Alhamisi, Mei 14, 2020 baada ya kutembelea mradi huo na kuzungumza na wananchi aliowakuta kwenye stesheni ya Soga, iliyoko wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Amesema faida nyingine ya mradi huo katika awamu yake ya kwanza, ni kupunguzwa kwa muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro. Amewataka wananchi hao wawe walinzi wa mradi huo kwa sababu utakapokamilika utawanufaisha na wao pia.

Reli hiyo itakuwa na vituo sita vya Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro, huku vituo vya Dar es Salaam na Morogoro vikiwa ndiyo vituo vikuu. “Kwenye vituo vya kushusha abiria vya reli hii, kutakuwa na huduma za kibenki na maduka, kwa hiyo wananchi hata kama hamsafiri, mtaweza kupata huduma na mahitaji yenu kutokea hapo,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages