A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 28, 2020

Trump kufanyia uchunguzi kifo cha Mmarekani mweusi aliyeuawa na polisi


Donald Trump amesema atapata ripoti "kamili" kuhusu kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa na polisi Minnesota nchini Marekani.

"Tutaangalia na tutapata ripoti kesho tutarudi. Tutapata ripoti kamili," Trump aliwaambia waandishi wa habari huko Florida.

Ameelezea mauaji hayo kama "tukio la kusikitisha sana."

George Floyd mwenye umri wa miaka 46 aliuawa mchana kweupe baada ya afisa polisi kumkamata na kumlaza chini kisha kumkaba shingo kwa kutumia goti lake.

Licha ya George Floyd kumuomba polisi msaada kuwa anashindwa kupumua,polisi huyo hakuliondoa goti lake mpaka pale mwanamume huyo aliposhindwa kuzungumza kabisa.

Gari la kubebea wagonjwa lilifika na kumchukua George Floyd ambaye bado alikuwa amekandamizwa na polisi huyo licha ya hali yake kuwa mbaya.

Iliripotiwa baadaye kuwa alifariki muda mchache tu baada ya kufikishwa hospitalini.

Wananchi wamekuwa wakiandamana wakitaka haki itendeke.

Maafisa wanne wamefukuzwa kazi kwa tukio hilo, ambalo limezua maandamano ya watu wengi na malalamiko dhidi ya ukatili wa polisi.

Ilhan Omar kwa upande wake amesema kuwa polisi huyo anapaswa kushtakiwa kwa kosa la mauaji.

Wanasiasa wengi na watu mashuhuri wamelaani kifo cha Floyd kwenye mtandao wa Twitter, na kusema ni "ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages