Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akisaini (mwenye miwani ) akisaini leseni ya MVIWATA FM Radio kulia ni Mhasibu Mwandamizi wa MVIWATA Thomas Tembe na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Sheria wa TCRA Vaolet Eseko katika hafla ya kukabidhiana Leseni ya MVIWATA FM Radio.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi leseni ya Radio Mhasibu wa MVIWATA FM Radio Thomas Tembe anayeshuhudia ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Sheria wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaolet Eseko katika hafla iliyofanyika ofisi ya kanda ya Mashariki TCRA jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKUU wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawaasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amewataka wamiliki wa vituo vya radio kufuata sheria ,Kanuni pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na Mamlaka hiyo ili kuweza kuhabarisha, kuburudisha na kuelelimisha wananchi kwa usahihi kwa mujibu wa masharti ya leseni wanazopewa.
Mhandisi Odiero ameyasema hayo wakati akikabidhi Leseni ya Kituo cha Radio cha MVIWATA kilichopo mkoani Morogoro. Amesema kuwa vituo vya radio lazima vizingatie Kanuni za Maudhui ya Utangazaji; bila kufanya hivyo mamlaka inaweza kuwafutia leseni zao.
Amesema kuwa wananchi wanahitakaji mambo matatu katika maudhui ya utangazaji ya ambayo ni Kuhabarishwa, Kuburudishwa na pamoja na Kuelimishwa hivyo kwenda tofauti na mambo hayo ni ukiukaji wa matakwa ya leseni.
Mhandisi Odiero amesema Mamlaka mpaka wanatoa leseni wanakuwa wameshapitia masuala yote muhimu iikiwemo mazingira ya studio pamoja na mitambo ya kurushia matangazo.
"Tunahakikisha wenye leseni za Utangazaji wanafuata miongozo yote ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika" amesema Mhandisi Odiero.
Kwa upande wa Mhasibu Mwandamizi wa MVIWATA FM Radio Thomas Tembe baada ya kupokea Leseni kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji MVIWATA radio Stephen Ruvuga amesema kua wanaishukuru TCRA kwa ushirikiano mzuri na ushauri mbalimbali walioupata tangu walipoanza maandalizi ya uanzishwaji wa radio hiyo.
Amesema watazingatia miongozo ya TCRA ya uendeshaji wa Radio pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na michezo na Sanaa ili kuhakikisha vipindi vyote vinajikita katika kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha.
Tembe alisisitiza kwamba MVIWATA FM Radio itahakikisha vipindi vyake vitawanufaisha Wakulima wadogowadogo , Wafugaji, wazalishaji wadogowadogo na Umma wa Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment