A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 4, 2020

SPIKA WA BUNGE NDUGAI AELEZA HALI YA MBUNGE ALIYEPATA CORONA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kuwa hali ya Mbunge wa kwanza aliyetangazwa kuwa amepata maambukizi ya Virusi vya Corona, inaendelea vizuri na kwamba hana dalili zozote za maambukizi hivyo anangoja vipimo vya mwisho ili aweze kuruhusiwa.

"Anaendelea vizuri hakuna mashaka yoyote, ila bado lazima zile siku za Karantini zipite, afanyiwe check tena na tena, lakini yuko vizuri kabisa kabisa na siyo kwamba aliugua, alikutwa na virusi katika wale ambao unaweza kupata Virusi lakini usiugue ama kuonesha dalili unawekwa tu mahali unapumzishwa na siyo kama anaumwa" amesema Spika Ndugai.

Aprili 20, mwaka huu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson, alitangaza kuwa mmoja wa Wabunge katika Bunge hilo amepata maambukizi ya Virusi vya Corona

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages