Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa ziara yake
yakukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk John Magufuli, katika Wilaya ya Kigamboni. Pia alikabidhi vifaa tiba kwa
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri kwaajili yakuanza kwa huduma kwa
hospitali mpya ya wilaya hiyo vikiwemo Magodoro 170, Mashuka zaidi ya 120 ndoo vyandarua na vingine vingi hafla hiyo imefanyika leo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri akizungumza wakati
wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Manispaa ya Kigamboni Ng’wilambuzu Ludga wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa kukagua miradi mbalimbali katika
Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa siku kumi kwa uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha Hospital hiyo inaanza kutoa huduma kwa wananchi ifikapo June Mosi baada ya Majengo yote ya Hospital hiyo kukamilika.
RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo pia amekabidhi Magodoro 175, Mashuka 1,294 na Ndoo na kueleza kuwa ifikapo Jumanne ya wiki ijayo atakabidhi tena Mashine mbili za Ultrasound zenye thamani ya Milioni 70 na Vitanda 100 ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa.
Aidha RC Makonda amemuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha anapeleka Watumishi 40 kwenye hospital hiyo kwaajili ya kutoa huduma ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Tano la kupunguza kero za Afya kwa Wananchi.
Akiwa katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara na Round about inayounganisha barabara za Kuelekea Feri na Kibada Kutokea Daraja la Mwalimu Nyerere RC Makonda amewaelekeza TARURA na TANROAD kuhakikisha ujenzi wa Barabara na Mzunguko wa Magari vinakamilika na kukabidhiwa kabla ya Mwezi September Mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa akiendelea na ziara akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri pamoja na viongozi wengine wa Serikali
Picha zote na Brian Peter
Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Jiji hilo kuhakikisha Maelekezo na Ahadi zote zinazotolewa na Rais Magufuli vinatekelezwa kwa Wakati pasipo kushurutishwa huku akiwataka Wakandarasi wote kuhakikisha miradi yao inakamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment