Na Amina Omari – Tanga
JESHI la Polisi mkoani Tanga linawashikilia vijana zaidi ya 30 kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya uhalifu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda alisema walikamatwa wakati wa oparesheni iliyofanyika wakati wa sherehe za Sikukuu ya Eid el Fitr.
Alisema siku ya Idd mosi walikamata vijana 20 na Idd pili walikamata vijana 10 ambao walikuwa na silaha kama mapanga.
“Vijana hawa walikamatwa wakiwa katika ugomvi wa makundi, baada ya wenzao wawili kugombana, kisha kutoa taarifa kwa wenzao na kusababisha ugomvi wa makundi,” alisema Kamanda Chatanda.
Alisema wakati wakitafutana ndipo walizua taharuki kwa wananchi kutokana na silaha walizokuwa wamebeba, ambao walilazimika kutoa taarifa polisi.
“Uhalifu huu unaweza kuleta madhara siku za usoni usipodhibitiwa, ni vijana wadogo, Jeshi la Polisi hatupo tayari kulea watu wenye nia ya kufanya vitendo vya kiuhalifu,” alisema Kamanda Chatanda.
Aliwataka wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya tabia za vijana wao kwani wakati mwingine wanajiingiza kwenye makundi ya uhalifu bila ya wao wazazi kujua.
“Kama katika hili la vijana hawa tuliowakamata, wengi wao ni wanafunzi na wazazi wao walikuwa hawajui kama wamejiingiza kwenye makundi ya uhalifu,” alisema Kamanda
No comments:
Post a Comment