A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 26, 2020

LIFEWATER INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA MASHINE ZA KUPIMIA SHINIKIZO LA DAMU KUKABILIANA NA CORONA

 Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety MalimaWa pili Kulia akimkabidhi Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile  Mashine’kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu ‘Corona’ leo Jumanne Mei 26,2020..Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wa pili kulia ni Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu ‘Corona’. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akifuatiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rose Malisa. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Afya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Rachel Kajobi.
Wa pili kulia ni Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile  na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rose Malisa Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu 'Corona'.
Muonekano wa Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ tano zenye thamani ya Shilingi Milioni 1 zilizotolewa Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu ‘Corona’.
Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile  akikagua Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ wakati Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akikabidhi mashine hizo kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu 'Corona'.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima (wa pili kulia) akizungumza wakati akikabidhi Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu 'Corona'.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (wa pili kushoto)  akilishukuru Shirika la LifeWater International kwa kutoa msaada wa Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Picha ya pamoja baada ya Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima (wa pili kulia). kukabidhi Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu 'Corona'.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la LifeWater International linalojihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira limetoa msaada wa Mashine za Kupimia Shinikizo la Damu ‘BP Mashine’ tano zenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya Mkoani Shinyanga ili kukabiliana na homa kali ya mapafu ‘Corona’.

Mashine hizo zimekabidhiwa leo Jumanne Mei 26,2020 na Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Malima amesema msaada huo ni mwendelezo wa mchango wa LifeWater International kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

“Leo tumetoa mashine ikiwa ni mwendelezo tu wa mchango ambao tumekuwa tukiutoa kwa serikali. Mtakumbuka hivi karibuni tulifadhili mafunzo kwa watoa huduma za afya na sasa tunaendelea kusaidia uhamasishaji katika halmashauri ya Shinyanga”,alisema Malima.

“Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano inaoendelela kutupatia. Tunaendelea kujipanga kuona namna gani tunaweza kueendelea kushirikiana na serikali zaidi ili kuhakikisha janga hili la Corona na wahudumu wanaofanya kazi hii wanafanya kazi katika mazingira rafiki,wanawasaidia wagonjwa na wao wenye wanabakia kuwa salama”,aliongeza Malima.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amelishukuru Shirika la LifeWater International kwa kuendelea kutoa mchango katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

“Tunawashukuru sana wadau wetu LifeWater International kwa kutupatia msaada huu wa Mashine za kupimia shinikizo la damu ‘BP Mashine’ ambazo zitatusaidia kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya sambamba na vile vituo ambavyo tumeainisha kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa Corona kama watatokea”,alisema Dkt. Ndungile.

“Mmefanya jambo zuri kutuletea BP Mashine kwa sababu magonjwa mengine pia yanakuwa na changamoto zake hasa unapotibu mgonjwa wa Corona, kwa hiyo vifaa hivi kwetu ni muhimu sana katika kuwahudumia wahisiwa wa Corona”,alisema Dkt. Ndungile. 

“Tunaomba wadau wengine waendelee kutuchangia kwani mapambano bado yanaendelea kwa hiyo lazima tuendelee kujiimarisha zaidi dhidi ya Virusi vya Corona. Bado mahitaji yapo,tunahitaji vifaa vingine kama hivi lakini pia mashine za kupimia wingi wa damu,wingi wa sukari mwilini na vifaa vya kujikinga”,aliongeza Dkt. Ndungile.


Naye Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Rose Malisa mbali na kulishukuru Shirika la LifeWater International pia aliomba wadau kuendelea kusaidia hospitali hiyo kwa kuipatia vifaa mbalimbali ikiwemo vipimo vya wingi wa hewa ya Oksijeni mwilini ‘Pulse Oxymetry’ ambavyo vimekuwa changamoto katika hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages