Beki kisiki wa timu ya Yanga Kelvin Yondani amekuwa kivutio kikubwa wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Sheria Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliokuwa wakifuatilia Mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha msaidi wa Yanga Charles Mkwasa, Yondani alionekana kufanya vizuri hasa alipokuwa akizuia mashambulizi ya timu pinzani iliyosheheni Mastaa washambuliaji wa timu hiyo.
Mkongwe huyo alionekana yuko fiti kwa kutimiza majukumu yote na kushiriki kikamilifu mazoezi yote magumu yaliyotolewa na Mwalimu Mkwasa.
Tangu kutua kwa Mwalimu Luc Eymeil Yondani amejikuta kwenye wakati mgumu kikosini humo huku akisugua benchi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu
No comments:
Post a Comment