A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 13, 2020

KAMPUNI YA MAGARI YA TATA YAPIGA JEKI SERIKALI YA MKOA KUPAMBANA NA CORONA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (watatu kushoto), akipokea mfano wa ufunguo wa kari kuashiria makabidhiano rasmi wa gari gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa kampuni ya 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (watatu kushoto), akipokea mfano wa ufunguo wa kari kuashiria makabidhiano rasmi wa gari gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa kampuni ya utengenezaji wa magari aina ya TATA, Thomas Macha na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RMO) ,Dkt. Rashid Mfaume


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) akipata maelezo kutoka ka Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya TATA Motors, Rajiv Bhushan wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RMO) ,Dkt. Rashid Mfaume pamoja TATA na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa kampuni ya, Thomas Macha. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo katika ofisi za Tata zilizobo vingunguti.


 Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu wa kampuni ya utengenezaji wa magari aina ya TATA, Thomas Macha, akizungumza wakati wa hiyo.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya TATA Motors, Rajiv Bhushan akizungumza katika warsha hiyo. Picha zote na Brian Peter



Kampuni ya Kimataifa ya Magari ya TATA Africa Holding Ltd leo imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo.

Gari hiyo aina ya XENON X2 Double Cabin RC Makonda ameelekeza itumike kuwasafirisha Watumishi wa Afya wanaofanya kazi ya Mapambano dhidi ya Corona.

Aidha RC Makonda ameishukuru kampuni hiyo kwa mchango walioutoa na kusema Gari hiyo itaenda kutatua changamoto za usafiri zilizokuwa zikiwakabili watumishi wa Sekta ya Afyahuku akieleza kuwa hali ya Maambukizi ya Corona katika Mkoa huo imepungua na Wagonjwa wengi wanazidi kupona.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya TATA Motors, Bwana Rajiv Bhushan amesema kwa siku ya leo wamekabidhi Gari moja ambapo Gari ya pili wataikabidhi muda wowote kuanzia sasa.

Aidha Bw.Rajiv amesema Kampuni hiyo imeona ni vyema ikawa sehemu ya mchango kwa jamii katika mapambano dhidi ya Corona kwa kuhakikisha watoa huduma wa Afya wanakuwa na usafiri wa uhakika.









No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages