Benki ya NMB na kampuni ya Savings at the Frontier (SatF) wamezindua huduma mahsusi kwa vikundi vya kuweka na kukopa nchini. Kwa ushirikiano huo, NMB na SatF zinakusudia kuwafikia zaidi ya vikundi 28,000 na wanachama wake walio nje ya mfumo rasmi na kuwaunganisha kwenye huduma za kifedha.
Mfumo huo mpya utatoa nafasi kwa vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na wanachama wao kutumia huduma za kidijitali za NMB zitakazowawezesha kufungua akaunti binafsi, kufungua akaunti za vikundi na kuweza kuzihudumia kupitia simu ya mkononi. Njia hii itawafanya wakidhi mahitaji ya wanachama bila kulazimika kukutana au kwenda tawi la benki na hivyo kutunza fedha kwa njia salama na ya uhakika.
Mfumo huu ni maboresho ya huduma ya ‘NMB Pamoja Account’ ambayo ni mahsusi kwa ajili ya Vyama vya Kuweka na Kukopa Vijijini (VSLA), Vyama vya Kijamii vya Akiba (SILC), Benki za Kijamii Vijijini (VICOBA), Vikundi vya Kijamii vya Akiba (CBSG), Mashirika ya Kijamii (CBO), Makundi ya Familia na Marafiki na kuyaunganisha na benki yenye mtandao mpana zaidi nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa NMB Pamoja Account, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema: “Lengo letu ni kuziba pengo lililopo kati ya taasisi za fedha na makundi yasiyo rasmi ya kuweka akiba na kukopa kwa kuyasogezea huduma za kibenki karibu yao. Huduma hii ambayo ni nyongeza kwenye NMB Pamoja Account, ni nafuu, inapatikana kila mahali na wakati wowote na ni rahisi kuitumia.”

No comments:
Post a Comment