MFANYABIASHARA maarufu nchini Rostam Aziz (pichani kushoto) akiwa sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda wakipita kwenye mashine maalumu za kupuliza dawa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa tukio akipokea msaada wa
vifaa vya kisasa vya kuwakinga wananchi wa mkoa huo dhidi ya
Virusi vya Corona vyenye dhamani ya zaidi ya shilingi Milioni mia 600 vilivyotolewa na Mfanya
Biashara maarufu nchini Rostam Aziz, vifaa hivyo vikiwemo mashine za kisasa 25 zenye uwezo wa kumtakasa mtu na kuuwa
vijidudu mwili mzima Barakoa 70,000 Dumu 600za ujazo wa lita 5 zenye Dawa
yakutakasa mikono pamoja na Santizer 600
Mfanya
Biashara maarufu nchini Rostam Aziz, akizungumza wakati wa tukio akikabidhi
msaada wa vifaa vya kisasa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, vya
kuwakinga wananchi wa mkoa huo dhidi
ya Virusi vya Corona vyenye dhamani ya zaidi ya shilingi Milioni mia 600 vifaa hivyo vikiwemo mashine za kisasa 25 zenye uwezo wa kumtakasa mtu na kuuwa
vijidudu mwili mzima Barakoa 70,000 Dumu 600za ujazo wa lita 5 zenye Dawa
yakutakasa mikono pamoja na Santizer 600
Rais wa
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dk Elisha Osati akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada
wa vifaa vya kisasa kutoka kwa Mfanya Biashara maarufu nchini Rostam Aziz,
kwaajili ya kujikinga na janga la Corona hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Karimjee posta Dar es Salaam Picha zote na Brian Peter
MFANYABIASHARA Maarufu Nchini Rostam Azizi chini ya Kampuni ya Taifa Gas leo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Shehena ya Vifaa vya Kisasa vya Kuwakinga Wananchi dhidi ya virusi vya Corona vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 600 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa Waziri Mkuu aliyoitoa wiki iliyopita ya kutoa Sh.bilioni moja kusaidia vifaa hivyo katika daladala za jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.
Vifaa alivyopatiwa RC Makonda ni Mashine za kisasa 25 zenye uwezo wa kumtakasa mtu na kuua vijidudu mwili mzima, Barakoa 70,000 Dumu 600 za ujazo wa Lita 5 zenye Dawa ya kunawa mikono pamoja na Sanitizer 600.
RC Makonda amesema Mashine hizo 25 zitapelekwa kwenye maeneo yenye msongamano wa watu kama Vituo vya Daladala na Masokoni na Dawa za kunawia mikono zitagawanywa kwa Watu wa Daladala kwaajili ya kuhakikisha kila abiria ananawa mikono.
Aidha RC Makonda amemshukuru Mfanyabiashara Rostam Azizi kwa upendo na moyo wa kuwajali wananchi wa Dar es salaam ambapo amesema atahakikisha kila kifaa kinamfikia mlengwa.
Pamoja na hayo RC Makonda amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya.
Kwa Upande wake Mfanyabiashara Rostam Azizi amesema ataendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo katika mambo mbalimbali ya kijamii ambapo msaada aliotoa keo ni mwanzo tu wa ushirikiano.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Rostam amesema pamoja na vitakasa mikono hivyo na Barakoa alizotoa lakini leo ameongeza mchango wake kwa hospitali mbalimbali kwa wauguzi wote ambapo amejitolea barakoa 70,000 ili madaktari na manesi ambao ndiyo wako hatarini kuliko mtu yeyote.
Vingine ni galoni 6,000 za lita tano za vitakasa mikono na mashine maalumu za kupuliza dawa ya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
“Kama nilivyosemna tuna janga. Janga hili la maradhi ya Corona haliko tu Tanzania lakini lipo sehemu zote duniani. Na kama sote tunavyojua ugonjwa huu hauna tiba, tiba pekee ni kujihami usiupate.
“Mheshimiwa Rais wetu Machi 22 mwaka huu, katika hotuba yake kwa taifa kuhusu janga hili, akitangaza maradhi ya Corona alitupa tahadhari, alituambia pamoja na kuchapa kazi na kuendelea na shughuli zetu za kila siku za kutafuta riziki lazima tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutokusanyika na mengineyo.
“Hivi sasa ni wazi kwamba tahadhari hizo inabidi tuzizingatie kuliko wiki iliyopita au wiki mbili zilizopita, leo hii kwa mara ya kwanza nimevaa hii kitu inaitwa barakoa na hii nimetengenezewa na mama yangu kwa hiyo huna haja ya kwenda kuinunua dukani unachukua shuka au foronya unaifunga na kamba,” amesema Rostam.
Akizungumza namna barakoa hiyo inavyofanya kazi, Rostam amesema inaweza kukuepusha na maradhi mengi, na kwamba jambo hilo linaweza kufanyika kwa kila mtu ambapo unaweza kuchukua nguo yako iliyochakaa ukatengeneza.
Amesema amezungumza na madktari wakamwambia ni vema kuvaa barakoa wakati unakwenda kwenye msongamano wa watu lakini pia watu wanaweza kutengeneza wenyewe si lazima kununua madukani.
Pamoja na mambo mengine, Rostam ametoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuisaidia serikali kwa kutoa msaada wa vifaa vya kupambana na corona akitolea mfano kwa nchi nyingine wafanyabiashara walivyosaidia nchi zao.
“Kama kawaida yangu ningependa kuwaomba wafanyabiashara wenzangu hili si jukumu la serikali pekee, wafanyabiashara wengi duniani wameishaidia serikali, tumeona Amazon wamejitolea. Si lazima uwe mfanyabiashara mkubwa, hata mfanyabiashara wa duka unaweza kuweka ndoo ya maji dukani na ukaweka vitakasa mikono kwa wafanyakazi unaweza kuokoa maisha ya watu.
No comments:
Post a Comment