A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, April 25, 2020

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani waanza



Ulimwengu wa kiislamu waanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, moja ya nguzo za imani ya uislamu.

Ijumaa katika mataifa kadhaa ulimwenguni tayari  waislamu wameanza  funga ya mwenzi mtukufu wa Ramadhani

Mwezi mtukufu wa Rmaadhani ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na waislamu kote ulimwenguni.

Waislamu katika pembe zote nne za dunia waliokuwa wakisubiri kuanza kwa mwezi mtukufu wameanza idadi ya mwezi huo katika kipindi ambacho kuna  maagizo tofauti katika juhudi za kupambana na virusi vya corona  ikiwemo marufuku  ya kutoka nje na mikusanyika ya umma.

Ikumbukwe kwamba katika mwezi mtukufu huo  hua ikishauriwa kwa waislamu kuchagia Iftar na wapita njia  au majirani, mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya corona , waislamu  hawoipata fursa hiyo ya  kujumuika  wakati wa iftar.

Kutokana na marufuku ya mikusanyiko , idadi ya  jamaa  katika miskiti pia ni marufuku katika mataifa tofauti kwa lengo la kuepukua maambukizi ya Covid-19.

Mataifa tofauti Mashariki ya Kati ikiwemo Uturuki   mikusanyiko ya umma kwa ajili ya ibada na iftar vimepigwa marufuku.

Nchini Indonesia, viongozi wa kidini wamewatolea wito waumini kubaki majumbani mwao na kufanyia ibada huku.

Nchini Saudia, kuingia na kutoka katika jiji la Makka na Madina  imepigwa marufuku.
Hija ndogo imesitishwa pia kutokana na janga a virusi vya corona.

Nchini Bangladesh,  kumechukuliwa hatua  ya kupunguza idadi ya watu  watakaokuwa wakiingia katika miskiti.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umeanza Aprili 24 , unatarajiwa kumalizika ifikapo  Mei 23 mwaka  2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages