Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
SIKU za hivi karibuni hasa wakati huu ambao dunia inapambana na mlipuko wa virusi vya Corona picha na video za kikundi hicho wakiwa wamebeba jeneza zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa ni kutahadharisha umma kuzingatia kanuni na sheria zinazotolewa na Wizara ya afya kabla ya kufikiwa na kundi hilo linaloshughulika na mazishi.
Kutokana na video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mtu anafanya kitemdo kinachohatarisha uhai wake na kuunganisha na video ya vijana ambao wanacheza kwa stepu moja huku wakiwa wamebeba jeneza.
Bila hiyana Michuzi Blog leo inawajulisha hao vijana ni akina nani na mwaka gani walianza shughuli yao ya kubeba jeneza na kucheza kwa stepu.
Mwaka 2010 Benjamin Aidoo raia wa Ghana alianzisha kikundi cha mazishi kinachofanya kazi ya kuzika wapendwa wa jamaa mbalimbali katika safari zao mwisho kwa namna ambazo jamaa hao watapendekeza hali iliyopelekea kikundi hicho kuwa maarufu sana barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla hasa kutokana na mtindo wanaotumia na nakshi wanazoweka katika shughuli za mazishi.
Benjamini aliwahi kufanya mazungumzo na kituo cha utangazaji cha BBC na kueleza kuwa kikundi hicho hufanya mazishi nchini Ghana na ameweza kuajiri watu wapatao 100 ili waweze kushirikiana naye.
Ameeleza kuwa wafanyakazi hao 100 wamepewa mafunzo mbalimbali ya maigizo na nakshi ambazo hutolewa kulingana na mahitaji ya wateja wao.
" Baadhi ya watu hupendelea maandamano ya heshima na wengine hupendelea ujuzi, harakati, na madoido yenye kuonekana hivyo nikaamua kuongeza vionjo ili mteja akija tunauliza anataka nini na tunafanya" alinukuliwa Benjamin.
Baadhi ya wateja wameeleza kuwa wamekua wakifuata huduma hiyo kutokana na mapendeleo ya wapendwa wao waliofariki.
"Baba alikuwa anapenda kucheza alipokuwa hai, leo acheze kwa mara ya mwisho" alinukuliwa mmoja ya wateja.
Benjamin alieeleza kuwa kucheza na jeneza wakati wa kuelekea kuzika ni mtindo mpya tofauti na ile ya kwenda taratibu.
Imeelezwa kuwa shughuli za mazishi nchini humo zimechukua nafasi kubwa kwa kupambwa na shughuli za mazishi
No comments:
Post a Comment