A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, April 25, 2020

IGP SIRRO AWATAKA WATENDAJI WA VIJIJI VILIVYOPO MIPAKANI KUDHIBITI WAGENI.

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Inspekta Simon Sirro amewataka watendaji wa Serikali za vijiji vilivyopo kwenye mipaka ya nchi kudhibiti Wimbi la wageni wanaoingia nchini kwa lengo kutafuta mahitaji ya chakula na baadhi ya bidhaa wakati nchi wanazotoka zimefunga mipaka zikizuia watanzania wasiingie kwa kuhofia maambukizi ya Covid-19 vinavyosababishwa na Virusi Vya Corona.

Amebainisha hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara baada ya kuzungumza na wakuu wa polisi mikoa ya kanda ya ziwa kwa lengo la kuimarisha usalama wa nchi.

Aidha Inspekta Simon Sirro ametoa onyo kwa wananchi wanaokaidi agizo la serikali kwa kuendelea kutumia mitandao ya Kijamii kupotosha takwimu za Virusi vya Corona hali inayosababisha hofu kwa jamii

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages