Charles James, Globu ya Jamii
WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu na vya kati jijini Dodoma wameishukuru serikali kwa kufunga vyuo hivyo ili kuondoa msongamano katika maeneo yao ya vyuo unaoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Wakizungumza na Michuzi leo jijini Dodoma wanafunzi hao wamesema kuwa ikitokea mmoja wao amekumbwa na virusi vya corona ingeweza kusambaa kwa kasi kubwa na kupelekea maambukizi kuenea kwa haraka zaidi hivyo serikali imefanya jambo la busara kufunga vyuo na shule za awali hadi Sekondari kwa simu 30.
Wanavyuo hao wamelalamikia adha ya usafiri wanayokumbana nayo hasa kwa wale wanaoenda mikoani ambapo magari yamekua machache kulinganisha na idadi ya wasafiri lakini pia nauli ikipandishwa kulingana na kiwango cha kawaida.
‘’ Kiukweli usafiri umekua changamoto sana kwetu unafika unakuta tiketi hazipo unashangaa magari yameisha ,unaambiwa kama unataka kuondoka ndani ya huo muda uongeze hela sasa kwa sisi tunaokaa mikoa ya mbali tunaangaika kwa kweli.
Mfano mimi kwetu ni Mkoa wa Mara nauli ya kwenda kwetu ilikua Sh 40,000 lakini sasa imepanda hadi 47,000 na wengine wanachaji hadi 50,000 jambo hili linatuwia vigumu sana na ndio maana toka jana tupo hapa," Amesema mmoja wa wanafunzi hao.
Ikumbukwe serikali imezifunga shule zote za kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita pamoja na vyuo vyote vikuu na vile vya kati kwa siku 30 hadi pale ambapo Wizara ya Afya itakavyotoa utaratibu.
No comments:
Post a Comment