A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 16, 2020

Tanga UWASA wapata changamoto mabadiliko ya sheria Na. 5 ya 2019




Na Rebeca Duwe, Tanga.



Kutokana na mabadiliko ya sheria ya Huduma za maji na usafi wa Mazingira  Na.5 Ya mwaka 2019 ,hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi imepungua kutoka aslimia 97 nakufikia asilimia 89   kutokana na  Tanga  UWASA  kuongezewa  na kuunganisha  eneo la kutolea Huduma ambapo kwa sasa  Tanga UWASA itahudumia kata zote 27 zinazounda jiji la Tanga , kata 6 katika mji wa Muheza kata  4 katika mji wa pangani .

Hayo aliyasema Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira jiji la Tanga Inj.Geofrey Hilly wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji yanayofanyika kila mwaka ambayo kwa mwaka huu yana kauli mbiu isemayo  “Maji Mabadiliko yaTabia Nchi;Uhakika wa Maji Salama kwa wote”  ambapo alisema mabadiliko ya sheria ya Huduma za maji na usafi wa mazingira  sheria Na. 5 ya mwa 2019  imesababisha kupungua kwa upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi kutoka  97%  nakufikia 87%  jambo ambalo ni changamoto kwa wananchi kupata huduma za majia kama walivyozoea.

Aidha  alisema katika kuhakikisha katika huduma inazidi kuimarika jumla ya miradi 18 imetekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016 mpaka sasa , kati ya miradi hiyo  10 inatekelezwa na wakandarasi na miradi 8 inaendeshwa kwa uwezo wa ndani ambapo utekelezaji wa miradi hiyo mpaka sasa umefanikiwa kwa 75%  ,miradi hiyo iko katika maeneo  ya  Tanga Jiji, Muheza , Songe , Lushoto, Mombo, Pangani , Horohoro, Mkinga na Kibinda.

Inj.Hilly  alisema pia Tanga  UWASA  kwa kushirikiana na umoja wa wakulima wahifadhi mazingira kihuhwi zigi (UWAMAKIZI)ina mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za uhifadhi mazingira na chanzo cha mto zigi ,jambo ambalo limesaidia wananchi kujua umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji kwa  mkulima  kuacha  mita 5 kutoka mtoni ambapo  anatakiwa alime mazao ambayo hayataathiri vyanzo vya maji kama Cocoa, pilipili manga , karafuu na mdalasini .

 Kwa Upande wake meneja wa Wakala wa usambazaji wa maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA)Inj. Upendo Lugongo amesema serikali inaboresha miundo mbinu ya maji na jumla ya bajeti bilioni 5 na mpaka sasa hivi  nusu ya pesa ya miradi imeshapatikana  na miradhi inaendelea kujengwa miradi  8 kwa nguvu ndani  ambapo Pangani miradi 5,Handeni mradi 1 na muheza miradi 2.

Aidha alisema lengo nikufikia asilimia 95 ya upatikanaji wa maji mjini na asilimia 85 vijijini ifikapo Juni 2020 ambapo mkoa wa Tanga kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji ni aslimia 57.2 ya watu ambapo ni sawa na idadi ya milioni 1 na laki 2 katika ya watu milioni 2 laki 2 walioko katika mkoa wa Tanga na wastani wa maji vijijini ni asilimia 52 na katika miji mikuu ya wilaya ni wastani wa asilimia 54 na Jiji la Tanga asilimia 89 ya watu wanaopata maji safi na salama.

Inj. Lugongo amesema kwa mkoa wa Tanga wako na wanajitahidi  kwa sababu miradi yote inaenda kutekelezwa kwa mapato ya ndani pamoja na wakandarasi watatumika kwa uchache ili wanancchi waweze kupata huduma kwa haraka lakini ndani ya muda mfupi ,hivyo katika kuhakikisha huduma ya maji inaendelea RUWASA ina majukumu yafuatayo , kusanifu na kusimamia miradi ya maji vijijini , kufanya utafiti kuhusu maji chini ya ardhi , kuchimba visima na kujenga mabwawa,kuasjili na kuviwezesha vyombo vy watumia maji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages