A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 19, 2020

SPIKA NDUGAI ASIMAMISHA ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUEPUKA CORONA, AZIRUDISHA DODOMA

Charles James, Globu ya Jamii

KATIKA kuhakikisha inafuata utaratibu uliotolewa na Wizara ya Afya kwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ameziagiza kamati zote za Bunge za kisekta kusitisha ziara zao.

Spika Ndugai amezitaka pia kamati hizo ambazo zipo kwenye mikoa mbalimbali nchini zikikagua miradi kusitisha ziara hizo na kurejea jijini Dodoma mara moja.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo, Spika Ndugai amesema kwa kipindi hiki kamati zitafanyika katika maeneo ya Bunge kwa zamu mchana na jioni ili kuzuia msongamano wa watu kama ilivyoelekezwa na Wizara ya Afya.

" Ninaziagiza kamati kurejea Dodoma na shughuli zote zitafanyika hapa bungeni, tayari tushachukua hatua za kuweka vitakasa mikono na vipima joto kwenye magari ya bunge lengo likiwa ni kuchukua tahadhari kuepuka maambukizi.

Pia kwa sasa pia tumechukua uamuzi wa kuzuia watu mbalimbali au vikundi ambavyo vimekua vikija kutembelea bunge kwa ajili ya kujionea shughuli zake," Amesema Mhe Ndugai.

Kuhusu ufanyaji wa kazi kwa sasa, Mhe Ndugai amesema shughuli nyingi za kuchambua bajeti kwa sasa zitafanyika kwa njia ya mtandao kwa kuwa kuna mtandao wa Bunge.

 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages