A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 9, 2020

SCANIA IKO TAYARI KULETA MABASI YANAYOTUMIA GESI YA ASILI NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund, akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund, akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scsnia iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam. Mwengine pichani ni Meneja Masoko wa Scania, Eliavera Timoth. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya  Scania Tanzania Ltd, Eliavera Timoth (kulia), akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scsnia iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu;

Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd yatangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus Rapid Transit). Bidhaa hii ni sehemu ya juhudi ya kampuni kuhakikisha inaongoza katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kampuni ya Scania inaamini kuwa ni wakati sahihi kwa Tanzania kuingiza katika mfumo huu na mingine kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu kimazingira na kiuchumi.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia na inahitaji maelfu ya mabasi ya jiji kwa mfumo wa BRT ambayo kampuni ya Scania inaweza kuleta. Kampuni ya Scania imekuwa imefanikiwa kuleta magari ya mfumo wa gesi kwa muda mrefu sehemu mbalimbali duniani kama Amerika Kusini, Ulaya na Australia.

Moja ya faida ya mabasi yanayoendeshwa na mfumo wa gesi asilia (Compressed Natural Gas) ni kwamba mfumo wake wa injini utasaidia kupunguza hewa chafu (Carbon dioxide) kwa asilimia 20 ambapo CO2 inatajwa kuwa ndio chanzo cha joto kali duniani, itapunguza gharama za uendeshaji, gharama kwa abairia na itasaidia serikali kuongeza mapato kupitia uuzaji wa gesi asilia.

Akizungumza na wanahabari katika ofisi kuu iliyoko Vingunguti kando na barabara ya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania, Lars Eklund amesema Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda, hivyo ufanisi unahitajika na kwamba mazingira yasisahaulike.

“Tunaamini ya kwamba Tanzania inahitaji kuwa na teknolojia mpya ili iendane na kasi ya nchi zilizoendelea. Tanzania ni tajiri sana kwa gesi asilia na ni muhimu kutumia nishati hii ya ndani kwa faida ya nchi, nchi itapata faida sana kwani itapunguza kiasi cha mafuta yanayoagizwa nje” na badala yake inaweza kuuza gesi ya ndani kwa waendeshaji wa ndani. Hakuna njia bora na ni ghari sana kujaribu kubadili injini ya dizel kuwa injini ya gesi. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kumekuwa na taaria kupitia vyombo vya habari kutaka kubadili mfumo wa sasa wa magari ya BRT kutoka injini ya dizel kwenda injini ya gesi, suala hili halina tija kiufundi na kiuchumi kwa sababu injini ya dizeli imeundwa kufanya kazi katika mzunguko wa dizeli wakati injini za gesi na petrol zinaendeshwa kulingana na kanuni ya Otto na ujazo wa kuziba cheche. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwepo kwa mipango bora ya upanuzi wa miundo mbinu ya gesi asili ambapo itasaida wauzaji na waendeshaji kuthubutu kuwekeza katika bidhaa sahihi za gesi asilia zitakazotumiwa barabarani haraka iwezekanavyo. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kama sehemu ya kukuza huduma zake nchini, kampuni ya Scania Tanzania inatafuta kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kufadhili wanafunzi wanaochukua elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia (Compressed Natural Gas). Hii itasaidia kuongezeka kwa idadi ya mafundi na wataalamu katika uwanja huo hivyo kuongezeka kwa msaada kwa watumiaji wa mabasi yenye mfumo wa gesi nchini. Mpango huu sio tu sehemu ya kujitolea kuboresha huduma lakini pia ni njia ya kurudisha fadhila kwa jamii zetu zinazotuzunguka. Alisema Bwana Eliavera Timoth, Meneja Masoko Scania Tanzania.

KUHUSU SCANIA TANZANIA LIMITED
Kampuni ya Scania Tanzania inafanya kazi kama kampuni ndogo ya Scana CV AB yenye makao makuu yake nchini Sweden. Kampuni ya Scania Tanzania inajihusisha na uingizaji na usambazaji wa bidhaa za Scania nchini. Kampuni hii ina ofisi sehemu mbalimbali nchini ambapo makao makuu yake ni Dar es Salaam, huku ofisi nyingine ni Mwanza, Arusha na Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages