A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 16, 2020

RC Makonda aagiza wamiliki wa mabasi kuweka maji ya kunawa na sabuni ili kujikinga na corona

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda ametoa agizo kwa  wamiliki wa mabasi makubwa na maodogo ya abiria  na uongozi wa stendi ya mabasi Ubungo kuweka sehemu za kunawa mikono kwa maji yanayotiririka ili kujikinga na corona.

“Wamiliki wote wa Mabasi makubwa na madogo ya kubeba abiria yanayoingia, kutoka na yaliyopo DSM, Boti za mwendokasi,Treni/TAZARA, Uongozi wa Standi ya Mabasi Ubungo n.k, nawasihi waweke sehemu za kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kwa sabuni ili kujikinga na corona”-Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda @baba_keagan •

“Katika kujikinga na virusi vya corona nawaomba abiria wote kabla ya kupanda na wakati wa kushuka katika vyombo vya usafiri, wasafishe mikono yao kwa dawa maalaum ya kutakasia mikono (Alcohol based Hand Rub Sanitizer)” - RC MAKONDA

“Kila taasisi ihakikishe uwepo wa dawa ya kutakasia mikono (Alcohol based Hand Rub Sanitizer), utekelezaji ukamilike kwa 100% ndani ya siku tatu kuanzia March 16, vyombo vya usafiri viepuke kujaza abiria zaidi ya uwezo (msongamano wa abiria ktk vyombo hivyo ni marufuku)”-RC MAKONDA

“Naelekeza uwepo wa ndoo za kunawia mikono zenye maji yanayotiririka na uwepo wa dawa za Kutakasia mikono kwenye hoteli, gesti, kumbi za starehe, Benki zote, ATMs, Bar, Clubs’, SuperMarkets/Malls, maduka, maeneo ya Ibada, Taasisi na Kaya zote n.k, ili kujikinga na corona”-RC MAKONDA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages