A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 16, 2020

Ndege ya Kenya yashindwa kutua Nairobi, yatua KIA kwa dharura



Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) iliyokuwa ikitokea Lusaka, Zambia kwenda jijini Nairobi, Kenya imelazimika kutua kwa dharura mkoani Kilimanjaro, Tanzania baada ya kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).



Ndege hiyo (KQ708) ilitoka Lusaka saa 9:35 alfajiri na ilitarajiwa kutua JKIA saa 1:35 asubuhi, lakini ilishindwa kutua kutokana na ukungu mzito uliokuwa umefunika uwanja.

Taarifa kutoka katika tovuti ya Flight Radar inaonesha kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua baada ya kujaribu kufanya hivyo mara mbili, ndipo ikaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages