Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amezindua huduma ya ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mtandao wa simu ya mkononi kupitia Airtel Money.
Uzinduzi wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya Airtel Money unarahisisha huduma hiyo ambapo wamiliki wa ardhi wataweza kufanya malipo kupitia mtandao huo wa simu bila kwenda ofisi za Ardhi.
Akizungumza jijini Dodoma jana tarehe 9 Septemba 2019 wakati wa kuzindua huduma hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema ubunifu wa serikali kufanya malipo ya Ankara za serikali kwa kutumia mfumo wa GePG umerahisisha malipo ya tozo mbalimbali za serikali ikiwemo kodi ya pango la ardhi.

No comments:
Post a Comment