Serikali ya Tanzania imesema imesitisha safari zake za ndege za Air Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo hadi pale watakapopata taarifa juu ya usalama wa abiria wao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa uzinduzi rasmi wa mamlaka ya hali ya hewa ya kubadirishwa kutoka wakala kwenda kuwa Mamlaka kamili, amesema hawawezi kuwapeleka abiria sehemu ambayo inamachafuko bila kujua usalama wao utakuwa vipi.
No comments:
Post a Comment