Awali Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa, Bweni na Matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Ulowa.
Serikali mkoani Shinyanga imewatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama juu ya uuzaji wa tumbaku kilo milioni mbili ambayo imebaki na kusema kwamba wanunuzi wapo na itanunuliwa yote.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Agosti 20.2019 katika viwanja vya shule ya Msingi Kangeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wakati wa ziara ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.
Telack amesema serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha kwamba wakulima hao wa tumbaku wanapata mnunuzi na tayari kampuni ya British American imekwishapatiwa kibali na itaanza kununua tumbaku hiyo hivi karibuni. "Kutokana na changamoto iliyojitokeza hapo awali ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutokana kampuni ya TLTC kusitisha ununuzi wa zao hili, serikali sikivu iliendelea kutafuta wanunuzi na tayari kampuni ya Alliance itanunua asilimia 10 ya tumbaku hiyo pamoja na kampuni ya British American ambapo yenyewe itanunua tumbaku yote itakayobaki",amesema Telack.
"Naagiza pia acheni kukata miti hovyo kwa ajili ya kuchomea tumbaku zenu ,nilishasema muwe mnakata matawi na siyo miti kama mnavyofanya hivi sasa na mkiendelea na hali hii nitasitisha ulimaji wa zao la tumbaku kwa sababu hatutaki tuishi kwenye hali ya jangwa,"ameongeza.
Aidha amewataka wakulima hao wa tumbaku kutumia vyema pesa ambazo watazipata kutokana na mauzo ya tumbaku, kwa kuzifanyia shughuli za maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao. Kwa upande wake, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema serikali ya Tanzania itawasaidia wakulima wa tumbaku ili kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa.
Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema kuwa shauku kubwa ya wakulima wa tumbaku wa kata ya Ulowa, ni kujua hatma ya uuzaji wa tumbaku yao iliyobaki yenye kiasi cha kilo milioni mbili na kumuomba mkuu wa Mkoa awapatie ufafanuzi wakulima hao juu ya suala hilo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga akiwatoa wasiwasi wakulima wa zao la tumbaku katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu kuwa serikali yao itahakikisha inawasaidia wakulima na kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa yote. Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kata ya Ulowa halmshauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao ni wakulima wa zao la tumbaku na kuwatoa wasiwasi kuwa tumbaku yao iliyosalia kilo Milioni 2 itanunuliwa yote. Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, alimuomba mkuu wa mkoa Zainab Telack kuwatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku juu ya hatma ya ununuzi wake mara baada ya kampuni ya awali iliyokuwa ikinunua zao hilo kusitisha ununuzi. Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Jimbo la Ushetu kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Elias Kwandikwa,ambapo alisema asilimia kubwa ya miradi ya maendeleo imetekelezwa ikiwamo ya huduma za afya , ujenzi wa zahanati, kituo cha afya , hospitali ya wilaya pamoja na unuaji wa vifaa tiba. Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Iddi, akiwataka wananchi wa kata ya Ulowa kuwa wawe wanachangia shughuli mbalimbali za maendeleo na siyo kutegemea kila kitu wafanyiwe na serikali, huku akitoa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 50 ili kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Ulowa. Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kangeme Kata ya Ulowa- Ushetu wilayani Kahama.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsalimia mmoja wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Ulowa Leticia Tungu (15) ambaye anasoma kidato cha kwanza. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Ulowa kusoma kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili waje kuwa tegemeo katika familia zao pamoja na taifa kwa ujumla kwa kupata watalaamu ambao watailetea maendeleo nchi. Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Mhe. Jumanne Kishimba akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Jimbo hilo, kuwa changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo ni ubovu wa miundombinu ya barabara hasa za mjini. Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba akikabidhi Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga. Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akiwaapisha wanachama wapya watano wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambao wamekihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
No comments:
Post a Comment