Wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga wanatarajiwa kumenyana katika kandanda safi la hitimisho la tamasha la mtaa kwa mtaa linalotarajiwa kutimua vumbi katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.
Tamasha hilo la aina yake linatarajia kuwakutanisha wakongwe hao wa kukinukisha, Agost 17 kabla ya AgostI 18 kupigwa fainali ya tamasha hilo iliyozishirikisha timu zaidi ya 100.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mashujaa, Maximilian Luhanga, amesema katika hitimisho la tamasha lao liloanza mwaka jana, wameamua kuwahita wakongwe hao wa soka ili kunogesha tamasha lao.
Amesema, siku ya hitimisho timu mbili zitamenyana katika mchezo huo wa fainali ambapo bingwa atazawadiwa gari aina ya Noah ambayo kwa imani yao itawasaidia katika kujiongezea kipato au timu kuitumia katika safari zao mbalimbali.
No comments:
Post a Comment