JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imepongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa nchi pekee ya SADC iliyoweza kufikia kiwango cha asilimia Saba (7) katika ukuaji wa uchumi wake mwaka 2018 kiwango kilichowekwa na SADC .
Pongezi hizo za SADC zimetolewa na Katibu Mkuu wake Dk.Stergomena Tax wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya hiyo ambao umehusisha wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.
Amefafanua nchi za SADC zimejiwekea lengo la kukuza uchumi na hivyo wameweka vigezo vya kuwa na uchumi mpana na Tanzania imetimiza vigezo hivyo na kuwa nchi ya kwanza kwa ukuaji uchumi ukilinganisha na nchi nyingine ingawa nazo zinapaswa kupongezwa kwani zinafanya vizuri.
"Nchi za SADC uchumi wake unakwenda vizuri sana na takwimu zinaonekana kwenda vizuri katika ukuaji wa uchumi.Hii imetokana na baadhi ya nchi kudhibiti mfumuko wa bei.
" Lakini naomba niseme kwa uchumi mpana wa SADC na nchi wanachama wanafanya vizuri na
Tanzania ni nchi pekee ambayo imefikia asilimia saba
ya ukuaji wa uchumi,"amesema Dk.Tax.
Wakati huo huo Dk.Tax alipokuwa anazungumzia mikakati ya jumuiya hiyo na hasa katika eneo la sekta ya nishati ya umeme,ametumia nafasi hiyo kuipongeza Tanzania kwa namna ambavyo imeamua kwa vitendo kuhakikisha inakuwa na umeme wa uhakika na unaojitosheleza.
Amesema wanaipongeza Tanzania kutokana na mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi unaendelea na kuongeza mradi huo utakuwa na tija kwa nchi za jumuiya hiyo kwani wanaamini utakaopatikana mbali ya kutumika Tanzania utaunganishwa katika nchi za SADC.
Baadhi ya Wakuu wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza leo Jumamosi Agosti 17, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa kikaomkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza leo Jumamosi Agosti 17, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakifuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza leo Jumamosi Agosti 17, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment