Rais
wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August
14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo
atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosia atawasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na
baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwaajili ya
kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wakuu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini Mwa Afrika SADC.
Aidha
RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini
kuanzia August 16 ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia
vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao.
No comments:
Post a Comment