A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, August 25, 2019

Mradi huu wa Maji kutumia Tsh. Milioni 300



Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (tanga Uwasa) imeeleza kwamba mradi wa maji eneo la Horohoro lililopo mpakani mwa Tanzania na Kenya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utagharimu kiasi cha milioni 300.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati alipotembelea na kukagua bwawa la maji eneo hilo wakati wa  makabidhiano ya mabomba 415 yenye thamani ya milioni 64.4 yatakayotumika kwenye mradi huo kwa uongozi wa serikali ya Kijiji cha Horohoro.

Alisema kwamba mradi huo ambao utakuwa ni kutoa maji kwenye chanzo cha maji ambao ni bwawa na kupelekwa kwenye tenki ambalo litakarabatiwa na kusambazawa kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha Horohoro ili kuweza kuondosha kero ya maji kwa wananchi.

Licha kutembelea bwawa hilo lakini pia alifika eneo ambako kunaendelea kujengwa kituo cha kusafishia maji kabla ya kuwafikia wananchi wanaoishi eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Hilly alisema kwamba alisema mamlaka hiyo wamepewa kazi na wizara ya maji kwa ajili ya kujenga mradi huo ambao utasaidia kuondosha shida ya maji.



Alisema kwamba hilo linatokana na eneo hilo kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa maji licha ya kuwa na bwawa ambalo lina uwezo wa kuhifadhi maji lakini wanapata maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu

Alisema kwamba mabomba hayo ni hatua mojawapo ya ujenzi mradi wa maji Horohoro kwa ajili ya kusafisha maji na kusambaza kwa wananchi pamoja na kituo cha Forodha kinachounganisha nchi ya Tanzania na Kenya kilichopo eneo hilo.

Aidha alisema kwamba sambamba na ujenzi huo lakini pia watawekwa vituo vidogo vya kuchotea maji (vioski) huku akieleza kwa mujibu wa takwimu za watendaji kwamba wananchi 5000 wanaishi maeneo hayo ndio watanufaika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages