Na John Luhende
Mwamba wa habari
Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Deugratius Francis Sangawe amewaomba wasamilia wema kumsaidia ,ili awezekupata namna ya kujipatia kipato baada ya kupata ajali ya pikipiki na kupata ulemavu wa kudumu.
Deuogratius alitoa ombi hilo katika mkutano wa kupongeza diwani wa kata ya vingunguti Omary Kumbilamoto pamoja na kutoa mafunzo kwa wajasiliamali ulioandaliwa na wanachi wa kata hiyo ,ambapo amemshukuru Kumbilamoto kwa msaada aliompa.
“Namshukuru sana Meya kwa moyo wake wa kujali mimi nilipata ajali miaka mingi nimekuwa ndani bila msaada sijiwezi kutembea leo amenipatia baiskeli (Wheel chair) itaniwezesha sasa kutekeleza majukumu yangu katika kufanya kazi maana mikono ninayo tatizo nimiguu”alisema
Katika mkutano huo Kumbilamoto ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Ilala ,amesema mkutano huo uliandaliwa bila ya yeye kuelezwa nini atafanyiwa na amewashukuru wananchi hao kwa moyo huo lakini naye aliandaa msaada baiskeli kwa mlemavu yenye thamani ya shilingi 400,000 pamoja na jiko la Ges .
“Nawashukuru sana wananchi wa Vingunguti sikujua kuwa jambo hili litakuwa kubwa namna hii,nashukuru kwa kunijali na kutambua mchango wangu ningali hai ,wengi tumezoea mtu anapo kufa ndiyo anakumbukwa “alisema
Hata hivyo Kumbilamoto amewataka viongozi nchini kuiga mfano wa uchapakazi wa Rais Magufuli ili kuleta maendeleo kwa taifa .
“Haya tunayafanya kumuunga mkono Rais wetu yeye hapumziki kuwatumikian watanzania hatabakiwa ameenda Chato kupumzika utasikia tu anafanya jambo fulani amekuwa mfano wa kuigwa ,tangu ameingia madarakani ametekeleza ahadi zake nyingi alizo waahidi watanzania “alisema .
Naye mwakilishi wa Boda boda kata ya vinguti alikuwa amemtaka kijana huyo kuichukulia hali yake kama fursa,na kusema kuwa kata hiyo imepata kiongozi mchapa kaqzi na anaye yali wananchi wake kwani amekuwa msaada kwa wananchi kwa kilajambo anapo hitajika .
“Sisi tumejaribu kwa kilahali kumsaidia mwananchama wetu baada ya kupata ajali lakini kipato chetu ni kidogo tunakila sababu ya kumshukuru Diwani kwa msaada mkubwa huu alio utoa na si tunaaahidi tutaendelea kusaidiana naye kwa kila hali”alisema mwenyekiti huyo.
Pamoja na hayo ,afisa Vijana Manispaa ya Ilala Sapicia Masaga ameahidi kumtafutia kikundi kijana huyo ili aweze kuunganishwa katika mikopo ya bajaji wanazo patiwa walemavu aweze kuendelea na kazi zakiuchumi.
“Usihuzunike sana kupata ulemavu siyo mwisho wa maisha Manispaa imekuona tua kuahidi kuwa hatutakuacha tutakuwa nawe begakwa bega nimekuona bado munao uwezo mkubwa wa kufanyakazi tena ulikuwa dereva tutakukopesha bajaji itakusaidia maana mikpo hii ya serikali haina riba natumani utaweza “alisema Masaga.
No comments:
Post a Comment