A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 9, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA IDARA YA AFRIKA YA IMF JIJINI DAR ES SALAAM

imf%2B%25281%2529
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
imf%2B%25282%2529
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
imf%2B%25283%2529
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
imf%2B%25284%2529
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie na ujumbe wake pamoja na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto james na maofisa wa Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
imf5
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019
imf6
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie akiongea na wanahabari akiwa na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na maofisa wa Wizara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 6, 2019

Baada ya mazungumzo hayo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewahakikishia Watanzania kuwa wizara yake imejipanga kutoa ufafanuzi wa maeneo yote ambayo yanapaswa kuwemo katika taarifa yaIMF ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ikiwemo utelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi.

“Ili uchumi wa nchi ukue ni lazima uwe unawekeza, na bahati nzuri sana Mhe. Rais amemueleza mgeni wake jinsi tunavyowekeza kwenye miundombinu hususani ujenzi wa reli ya kati, jinsi tunavyowekeza katika ujenzi wa bwawa kubwa litakalotupatia megawati 2,100 za umeme na pia miradi ya barabara na viwanda vingi vilivyojengwa, haya ndio yanayokuza uchumi na sisi tunaamini kabisa wenzetu hawakuyazingatia kabisa katika taarifa ya awali (iliyovuja)” amesema Dkt. Mpango.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amewatoa shaka wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuendelea kuwa na imani na mazingira ya uwekezaji ya Tanzania na amewataka Watanzania kutokua na hofu kwamba wawekezaji watapungua kwani wawekezaji hao wanaendelea kuja.

“Nashukuru kwamba hata wawekezaji wenyewe hawana hofu kwani hata baada ya taarifa hiyo kuwa imevujishwa bado wengi wameendelea kuja na kuonesha nia ya kufanya kazi na sisi, na nashukuru Shirika la Fedha la Kimataifa kwa kuja kuzungumza na sisi, hiyo ni dalili kuwa shirika hili bado lipo nasi na bado tunaendelea na mazungumzo" Amesema Prof Kabud na kuongeza kuwa "Wale ambao walidhani pana ugomvi mkubwa kati ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Tanzania walikuwa wamekosea kabisa,na msimamo wa Tanzania utafahamika baada ya mazungumzo kuanza na kuweza kuwapitisha katika miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inafanyika” amesema Prof. Kabudi.

Kwa upande wake Selassie amesema aliomba kukutana na Rais Magufuli ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na IMF na jinsi shirika hilo linavyoshiriki katika kutoa ushauri wa kiuchumi.

Selassie amempongeza Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa juhudi kubwa zinazofanywa kuwekeza katika miradi mikubwa ikiwemo miundombinu itakayopunguza gharama za nishati ya umeme.

Kuhusu kuvuja kwa taarifa za ukuaji wa uchumi, Selassie amesema IMF itatuma timu ya wataalamu wake itakayokutana na timu ya wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango ya Tanzania kwa lengo la kupitia maeneo yote yaliyoanishwa katika matazamio ya ukuaji uchumi ya IMF na yale ya Serikali ya Tanzania.

“Mimi na Rais Magufuli tumekubaliana kuwa IMF na Tanzania watabaki kuwa wadau wanaoaminiana, tunaona fursa nyingi na muhimu katika nchi hii ikiwemo mipango mizuri ambayo Rais Magufuli ameianzisha.” Amesema Selassie na kuongeza kuwa


“Katika wiki zijazo, tutaendelea na mazungumzo na kuendeleakufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania na tutaleta timu ya wataalamu watakaokuja kujadiliana na Serikali ya Tanzania ili kutazama maeneo yote yaliyofanyiwa mageuzi makubwa na kuyawianisha na ukuaji wa uchumi” amesema Selassie. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages