A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 1, 2019

Mwanafunzi wa kidato cha pili ajinyonga Mwanza


Na James Timber-Mwanza

Mwanafunzi Masumbuko Kaselya (23) aliyekuwa anasoma  kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Nyakasungwa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amejinyonga baada ya kufanya mtihani wa majaribio wa kujiandaa na Mtihani wa Taifa.

Mkuu wa shule ya Sekondari Nyakasungwa   Erikana Mashimba  alisema kuwa siku  ya Aprili 30 mwaka huu walikuwa na mitihani  ya  majaribio  ghafla mwanafuzni huyo alitoweka alitoweka na Majira ya saa 11 jioni walipata taarifa ya kukutwa mwanafunzi huyo amejinyonga kwenye juu ya  mti.

Aidha Mwalimu alieleza kusikitishwa na kifo cha  mwanafunzi huyo kwani alikuwa ni moja kati ya wanafunzi waliokuwa wanaongoza kwa kufanya vizuri shuleni hapo ambapo hadi sasa ameshindwa hata kuelewa ni kitu gani kilichomsibu mpaka akachukuwa maamuzi hayo magumu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho  Bulumba Selestini Kamondo alisema kuwa alipata taarifa kwamba kuna mwanafunzi amejinyongwa kwenye mti ambapo alifika katika eneo hilo lakini alikuta tayari amefariki.

Aidha Mkuu wa Wiilaya ya Sengerema Emmanuel  Kipole aliwataka wazazi kuhakikisha wanafuatilia watoto wao katika masomo na kushirikiana nao kwa kila jambo ili kujua maendeleo yao jambo litakalowaondolea msongo wa mawazo na kujiepusha na maamuzi yasiyofaa.

Kipole alitoa rai kwa wanafunzi kujitika katika elimu kwani ndio mkombozi wao na kuavhana na  maamuzi yasiyofaa yanayogharimu wazazi, na kuahaidi kutoa taarifa pindi uchunguzi utakapokamilika ili kubaini chanzo cha kifo chake.

Mmoja ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakasungwa Baraka Boniphace anayesoma kidato cha tatu alisema kuwa kujinyonga kwa mwanafunzi mwenzao kumeleta simanzi kuwa na kuwaweka katika wakati mgumu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages