Kampuni ya mawasiliano ya simu, Tigo, imezindua mnara wa 3G katika kata ya Kidete, mkoani Iringa kama moja ya jitihada zake za kufikisha huduma bora za kupiga na kupokea simu, intaneti na kutuma na kupokea pesa kwa wateja wake.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.
Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa agenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi.
Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdurahamani, alisema kwamba kipaumbele ya Tigo ni kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.

No comments:
Post a Comment