A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 17, 2019

WATEJA WA TIGO MIKOA YA MBEYA NA IRINGA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa, Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya namna mteja anavyoweza kutumia simu yake kufanya malipo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo, Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa.
Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya. Kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na kushoto ni . Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo.
Waandishi wa habari wakimskiliza Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni . Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Kadri Makongwa.
Fanya malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama kwa zaidi ya idara 300 za Serikali, mawakala na mamlaka mbali mbali kupitia Tigo Pesa
Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Mbeya na Iringa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (WSSA) Afisa Uhusiano Msaidizi wa WSSA Mbeya Kadri Makongwa, alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka(WSSA)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages