A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 19, 2019

RC Rukwa awaonya walioshambulia gari la Serikali


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewaonya wananchi wa Kijiji cha Nankanga, Kata ya Nankanga, Wilayani Sumbawanga kuacha tabia ya kuharibu mali za serikali ili kutafuta suluhu ya migogoro.

Imeelezwa kuwa kumekuwa na migogoro kati yao na askari wa hifadhi ya Pori la Akiba Uwanda katika bonde la ziwa Rukwa.

Ametoa maagizo hayo baada ya gari ya hifadhi hiyo kushambuliwa na wavuvi waishio katika kambi ya uvuvi ya Kijiji cha Nankanga kilichopo pembezoni mwa ziwa Rukwa, tukio lililotokea April 10 mwaka huu.

Wavuvi hao walivunja vioo vya gari, kuchomoa tairi pamoja na kuchukua vitu vilivyokuwamo ndani ya gari huku dereva wa gari hiyo kukimbia na kuicha gari hiyo. Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amemuagiza kamanda wa Polisi Mkoa kuwasaka na kuwakama wote waliohusika na uharibifu huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages