A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 17, 2019

RC MAKONDA aweka jiwe la Msingi ujenzi wa madarasa na mabweni Shule ya watoto wenye ulemavu wa macho.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi, wakati Mkuu wa Mkoa alipokwenda kukagua miradi mbalimbali katika Wilaya hiyo leo. wengine pichani ni baadhi ya viongozi wanaosimamia miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Madarasa,Mabweni,pamoja na Vyoo mahususi kwa watoto wenye ulemavu wa Macho pekee katika shule ya msingi Toangoma iliyopo katika halmashauri ya Temeke ikiwa ni Shule ya kwanza katika Mkoa huo.
Rc Makonda ameweka jiwe hilo  Leo alipokuwa katika mwendelezo wa ziara  ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo ametembelea baadhi ya miradi katika halmashauri ya wilaya ya Temeke, Ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara, ujenzi wa vyoo, madarasa pamoja na mabweni katika shule ya msingi Toangoma itakayokuwa maalumu kwa watoto wenye ulemavu wa macho.
Amesema shule hiyo itatoa nafasi ndani ya Mkoa pamoja na nje ya mkoa ambapo  itakuwa Shule ya Kwanza Katika mkoa huo ya watoto wenye ulemavu wa macho hivyo ametoa wito kwa wazazi kutowaficha ndani watoto badala yake wawapeleke shule ili kuweza kupata elimu maana ni haki ya kila mtoto kupata elimu.
“Hongereni sana kwa kazi nzuri hiki mlichokifanya mtawasaidia wana Temeke mtawasaidia wana Dar es Salaam lakini pia mtalisaidia Taifa kwa Jumla, tuna fahamu changamoto kubwa sana kwa walemavu ni Elimu mlichokifanya sio tu Maendeleo lakini pia mmetekeleza hata maandiko matakatifu" Amesema Makonda.
Pia ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kisima unaotarajiwa kukamilika mei mwaka huu kilichoko katika Kata ya Charambe, pamoja na kituo cha Afya cha Ghorofa 3 kilichopo katika kata ya Yombo.
Aidha amepongeza uongozi wa manispaa hiyo kusimamia kikamilifu miradi ya Maendeleo ambapo wamepiga hatua kubwa hasa Katika ujenzi wa Barabara zenye viwango na kwa gharama ya chini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu matumizi ya fedha katika ujenzi wa shule ili kuhakikisha inakamilika kwa muda muafaka, amesema Mpaka saa ujenzi wa Bweni hilo na madarasa yamefikia 97%  ili kuweza kukamilisha ujenzi huo, ambapo amesema Bweni hilo litabeba Jumla ya watoto 80 na kusema kwasasa katika shule hiyo ina watoto 24.
Amesema lengo si kuangalia wenye ulemavu wa macho tu bali ni kugusa watoto wote wenye ulemavu wa viungo na kuhakikisha wanapata elimu, pia ametoa shukurani kwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kusimama na kuwasaidia kila wanapohitaji msaada wa Maendeleo katika halmashauri hiyo.
“Kwasasa tumeanza na jengo litakalo hifadhi jumla ya watoto 80, tuna mpango Mungu akipenda tutaendelea zaidi lento letu ni kuhakikisha tunatoa nafasi kwa watoto wote wenye matatizo ya viungo mimi kama Mkurugenzi naahidi nitapambana hadi senti ya mwisho nikishirikianana Rais wangu Dkt. John  Magufuli” Amesema Mwakabibi.
Ujenzi wa shule hiyo ya walemavu unatarajiwa kugharamia kiasi cha shilingi milioni 120 kwa majengo matano na kwamba mpango mkakati uliopo ni kuhakikisha wilaya ya Temeke inajenga takribani shule tano za watu wenye ulemavu

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages