A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 23, 2019

RC MAKONDA AKOSHWA NA KASI YA UJENZI WA MIRADI ILALA.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(katikati) wakikagua barabara ya Mtaa wa  Kiwalani Dar es Salaam leo katika ziara yake ya kikazi Wilayani Ilala, ( kushoto) ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (wapilikushoto) akimsikiliza Mhandisi wa ujenzi wa soko la Kisutu Taher Jafferji (wapilikulia) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kukagua miradi mbalimbali katika wilaya hiyo leo. kushoto ni Afisa Elimu Mkoa Hamisi Lissu
 Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda akisalimiana na mmoja ya wakazi wa kiwalani wakati  ziara ya kikazi Wilayaya Ilala (kulia) ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala pia ambae ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto.
  Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikiliza  mmoja ya wafanya biashara wa  Kariakoo mtaa wa Gerezani wakati  ziara ya kikazi Wilayaya Ilala (kulia) ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala pia ambae ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto.






 Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(katikati) wakikagua barabara ya Mtaa wa  Gerezani Kariakoo Dar es Salaam leo katika ziara yake ya kikazi Wilayani Ilala, ( kulia) ni Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto.
 Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Mabioresho ya Hospitali ya Mnyamani Buguruni.

 Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema wakikagua ujenzi wa hospitali inayojengwa Kivule .

MKUU wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda,amempongeza Kasi ya Ujenzi wa hospitali ya Kivule iliyopo Katika Wilaya ya Ilala.

RC Makonda amefikia hatua hiyo Mara baada ya kufanya Ziara Katika Wilaya hiyo na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ambapo amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa kivule, Ujenzi wa Soko la kisasa kisutu, Hospitali ya Buguruni, Barabara ya Kiwalani Pamoja na Barabara ya Gerezani ambayo ni miradi mkakati.

Amesema mradi wa Ujenzi wa hospitali ya Wilaya inategemewa kukamilika mwezi June mwaka huu ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kukahakikisha anaendelea kuusimamia vyema.

" Kwanza kabisaa nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kusimamia vyema ujenzi wa hospitali hi ya Kivule Kasi wanayoenda nayo Ni nzuri na matumaini yangu Hadi kufikia June 30, mwaka huu utakuwa umeisha" Amesema Makonda.

 Ameongeza kuwa miradi yote hiyo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwa lengo la kuwasaidia wanyonge ambao Ni wananchi wa hali ya chini.



Amesisitiza kwamba Rais John Magufuli anataka kuona huduma zinamfuata mwananchi na siyo mwananchi anaifuata huduma na kuongeza kwamba hospitali hiyo itatumika kwa wananchi wote ambao walikuwa wakienda  kufuata huduma katika Hospitali  ya Amana ambao wanaoshi maeneo hayo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo  amesema watu waache dhana kwamba Kuna watu wanaotumia wanyonge kwa manufaa yao binafsi kwani Katika Serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kuwainua na kuwatetea wananchi wanyonge.

MATUKIO KATIKA PICHA





















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages