Na, Editha Edward-Tabora
Watu Watano wa Familia moja katika kijiji cha Isonge Kata ya Sikonge Mkoani Tabora wameuawa na watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na Mvua na Upepo mkali
Tukio hilo lililoibua simazi kubwa limetokea usiku wa saa tano katika kijiji hicho
Nae kaimu Mathew Sipemba ni kaimu Mganga Mfawidhi Wilaya ya Sikonge amesema alipata taarifa hiyo kutoka polisi juu ya tukio hilo na kukuta watu Watano walikuwa tayari wamepoteza maisha
"Ajali ya radi sio nzuri ni kama moto watu hawa wamejikuta wanavuta hewa ya harufu kali na kuunguza mapafu jambo ambalo limepelekea kupoteza maisha kwa watu hawa"Amesema Sipemba
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina msaidizi Emmanuel Nley amesema Radi hiyo ilisababisha ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala familia hiyo kupasuka na kusababisha vifo hivyo
"Nyumba Ilikuwa imejengwa kwa udongo na makuti na kuezekwa kwa nyasi Mvua iliponyesha ilisababisha ukuta kupasuka na kupelekea tukio hilo kutokea "Amesema Nley
Kamanda Nley amesema katika tukio hili waliopoteza maisha ni Mhindi Peter, Vailleth Juma, Gress Juma Kulwa Lukanya na Nyanzobe Juma
Peter Nzalalila ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge amesema tukio hili lkmeibua simanzi kubwa na amewataka Wananchi wa eneo hilo kuacha kuhusisha tukio hilo na Imani za kishirikina.
No comments:
Post a Comment