NA HERI SHAABAN
KITUO chaTaarifa, na Maarifa cha Sayari kilichopo mtaa wa Gogo Kata ya ZINGIZIWA wilayani Ilala, kimetoa mafunzo ya elimu ya upambaji kwa wanachama wake.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yamefunguliwa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa serikali za mitaa Gogo Ramadhan Mapunda .
Akifungua Mafunzo hayo ya upambaji Mapunda aliwataka wanachama wa kituo cha Taarifa na Maarifa cha Sayari kufanya kazi za jamii kwa kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali.
"Nimefarijika leo kuwa mgeni rasmi katika mafunzo haya ya wiki mbili elimu mtakayo pata katika mafunzo haya itawafanya muwe Wajasiriamali bora katika kituo cha Sayari pamoja na Kata ya ZINGIZIWA kwa ujumla"alisema MAPUNDA..
Mapunda aliwataka wanachama wa kituo hicho cha sayari kuishirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.
Aliwataka washiriki katika kazi za kijamii na kushirikiana na serikali ya Mtaa hadi ngazi ya Kata kwa kila jambo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Nipael Joshua alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanachama 19 kwa sasa 76 kinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.
Nipael alisema Kikundi cha Sayari kinashughulika na kilimo ,utengenezaji wa Batiki, Sabuni za maji.
Dhumuni la kuanzishwa kwake ni kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kuacha maisha tegemezi.
Akielezea dhumuni la kituo hicho kuboresha UCHUMI wa afya na kuisaidia watoto walio katika mazingira hatarishi.
Pia kutoa elimu ya Mambo ya jinsia sambamba na kuwahudumia watoto waliokuwa katika mazingira magumu kwa mfano kwa sasa kituo hicho kina kinamuhudumia mwanamke mmoja ambaye alipokelewa akiwa na ujauzito na sasa amejifungua akiwa kituo hicho baada mwanaume kumtelekeza.
"Sisi kama Sayari kituo chetu ni cha kijamii kina shughuli nyingi zikiwemo kupinga rushwa ya ngono na kupinga utekelezaji katika JAMII "alisema Joshua.
No comments:
Post a Comment