Na. Enock Magali,Dodoma
Wakala wa majengo nchini (TBA), imekamilisha ujenzi na kukabidhi rasmi majengo ya Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala bora waliyokuwa wakiyajenga katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma
Mradi huo wa ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo ulianza mnamo Disemba 26 mwaka 2018 ambapo ulianza kwa kazi ya usanifu iliyofanywa na idara ya ushauri ambapo mara baada ya hapo ujenzi ulianza ukikihusisha kikosi cha ujenzi kutoka TBA
Akizungumza wakati akikabidhi majengo hayo March 22 mwaka huu mbele ya Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mh,George Mkuchika,Mkurugrnzi kutoka TBA Humphrey Kilo amesema hadi sasa zaidi ya Shilingi Milioni mia tisa imekwisha tumiak katika ujenzi huo ambayo ni gharama ya chini kutokana na kubana matumizi ili kuweza kufikia malengo ya bajeti iliyotolewa
“Mpaka tarehe ya leo tumekwisha kamilisha kazi zote zilizopo kwenye mkataba wetu ,na kwa ubora na leo tumekabidhi,kazi nyingine zilizobaki ni za usafi na kazi nyingine za kuborsha mazingira kama unavyoona”Alisema
Kwa upande wake Waziri Mkuchika pamoja na kuwapongeza TBA kwa kukamilisha kazi kwa wakati pia amesema wao ndio Wizara ya kwanza kukabidhiwa majengo kwa wakati lakini pia watakuwa ndio Wizara ya kwanza kuhamia na hiyo ni ishara ya kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli ya kuhamia Dodoma hivyo kuwataka watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii
“Yote haya hayaoti tu kamaUyoga unavyoota Porini ,ni kwa jitihada na ufadhili wa Serikali yetu ya Awamu ya tano,inayoongozwa na Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli kupitia kodi za wananchi.kwa upande wetu sisi watumishi tunaweza kuendelea kumtia moyo kwa kuongeza bidii ya kuchapa kazi na kuwahudumia watanzania”Alisema
Sambamba na hilo pia Waziri Mkuchika amekabidhi hati ya viwanja kwa baadhi ya watumishi wa wizara hiyo waliohamia Dodoma ambapo kufuatia hilo amewapongeza watumishi hao kwa kusema kuwa wameonyesha uzalendo na ni mfano wa kuigwa
Aidha Ofisi hizo zinatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi April 02 mwaka huu ambapo wananchi wote watakao hitaji huduma kutoka katika ofisi hizo watalazimika kuzifaya katika mji wa Kiserikali
No comments:
Post a Comment